Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 05:21

Marekani na Norway watishia kuwekea Sudan vikwazo


Waandamanaji wakiwa kwenye mji mkuu wa Khartoum kwenye picha ya awali
Waandamanaji wakiwa kwenye mji mkuu wa Khartoum kwenye picha ya awali

Marekani, Norway, Uingereza na Umoja wa Ulaya Jumanne wameonya utawala wa kijeshi wa Sudan kwamba hawataunga mkono waziri mkuu mpya iwapo washika dau mbali mbali wa kiraia hawatahusishwa, wakati pia wakitishia kuweka vikwazo vya kiuchumi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taarifa kutoka kwa mataifa hayo yanayojulikana pia kama ya Troika na EU imesema kwamba kuna umuhimu wa kubuniwa kwa serikali yenye hadhi pamoja na bunge ili kuendelea kupokea misaada ya kifedha.

Taarifa imeongeza kusema kwamba mataifa hayo yatawajibisha wale wanaohujumu mchakato wa demokrasia, iwapo hakuna hatua zitakazopigwa.

Onyo la Jumanne limekuja siku mbili tu baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu Abdalla Hamdok ambaye alikuwa ameshikilia wadhifa huo tangu mwaka wa 2019, na kuondolewa Octoba 25, mwaka jana, baada ya mapinduzi ya kijeshi na kisha kurejeshwa Novemba 21, kupitia mkataba uliopingwa vikali na wanaharakati wa demokrasia.

Mataifa ya Troika pia yamesema kwamba, “Watu wa Sudan wamezungumza kwa sauti inayoeleweka sawa na mwaka wa 2019,kwamba wanapinga utawala wa kidikteta na wangependa mpito kuelekea utawala wa demokrasia uendelee. Ni jukumu la viongozi walioko sasa kuonyesha kwamba wamesikia.”

Wakati wa kujiuzulu , Hamdok alitetea hatua yake kwa kusema kwamba alishindwa kuleta pamoja makundi yanayotofautiana kuhusu mpito baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al Bashir, Aprili 2019.

Marekani, Norway, Uingereza na UE sasa wanasema kwamba kunahitajika kuwepo viongozi wa kiraia watakaokamilisha majukumu ya mpito yaliyopo, yakiwemo maandalizi ya uchaguzi pamoja na kubuniwa kwa mihimili ya serikali, bunge na mahakama.

XS
SM
MD
LG