Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 05:31

Maandamano mengine yaitishwa na kamati ya upinzani Sudan

Muandamanaji akibeba picha ya Waziri Mkuu Abdall Hamdok wakati wa kupinga utawala wa kijeshi
Muandamanaji akibeba picha ya Waziri Mkuu Abdall Hamdok wakati wa kupinga utawala wa kijeshi

Duru ya 13 ya maandamano tangu mapinduzi ya kijeshi tarehe 25 Oktoba, yaliitishwa na kamati ya upinzani katika mji pacha wa Omdurman wa Khartoum kujibu mauaji ya waandamanaji kadhaa siku ya  Alhamisi na Jumapili.

Maandamano yanafanyika siku mbili baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, ambaye alihudumu kutoka Mwaka 2019 hadi mapinduzi na kurejeshwa tena Novemba 21 katika makubaliano na jeshi yaliyopingwa kwa kiasi kikubwa na waandamanaji.

Takriban watu 57 wameuwawa katika maandamano hayo ya kupinga utawala wa kijeshi tangu Oktoba, kulingana na madaktari.

Katika wiki za hivi karibuni, waandamanaji wamelenga ikulu ya rais mjini Khartoum, huku umati wa watu kutoka Omdurman na Bahri, ng'ambo ya Mto Nile kutoka Khartoum, wakijaribu kuvuka madaraja.

Kwa kujibu hayo wanajeshi siku ya Jumanne walifunga madaraja kadhaa na barabara kuu. Nazo kamati za upinzani zilizoandaa maandamano hayo ziliwaelekeza watu mbali na madaraja hayo.

XS
SM
MD
LG