Mtu yeyote ambaye si raia wa Marekani aliyekuwa katika moja ya nchi nane katika siku 14 kabla ya kuja Marekani atazuiliwa kuingia nchini.
Masharti hayo hayatawahusu raia wa Marekani na wale wenye ukazi wa kudumu; hata hivyo, watatakiwa kupimwa na kubaini kuwa hawana maambukizi kabla ya kusafiri, kama itakavyowalazimu wasafiri wote wa kimataifa.
Biden alitoa tangazo hilo Ijumaa baada ya kushauriana na Dkt Anthony Fauci, mshauri wake mkuu wa masuala ya afya.
Mbali na Afrika Kusini, nchi nyingine ni Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji na Malawi.
Biden amechukua hatua hiyo baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza aina mpya ya virusi, B.1.1.529, virusi vilivyotia wasiwasi na kuviita ni omicron.
Katika tangazo lake, Biden amesema alikuwa na ujumbe muhimu kwa watu Wamarekani: Kwa wale waliokamilisha chanjo, “ nendeni mkapige chanjo ya ziada mara tu itakapokuwa muda wako umefika.” Na wale ambao hamjakamilisha chanjo, kachanjeni hivi leo.”
Ni Nini Omicron
Omicron ni aina ya tano ya virusi vilivyotangazwa na WHO kuwa vimeleta wasiwasi. Mara ya kwanza viligunduliwa katika wiki za karibuni huko Afrika Kusini, vimeonyesha ongezeko la kasi kubwa kwa maambukizi ya COVID-19.
Kuna kiasi cha mabadiliko 30 ya virusi vinavyoshambulia vyenye asili ya protini, na wanasayansi wana wasiwasi kuwa baadhi ya virusi hivyo vinaweza kuwa rahisi sana kusambaza maambukizi. Lakini wana sayansi hawajaweza ufahamu iwapo omicron ni yenye maambukizi zaidi au hatari sana.
Wasiwasi juu ya aina mpya ya virusi vimepelekea masoko ya fedha kuanguka Ijumaa na kushusha bei ya mafuta ghafi kufikia dola 10 kwa pipa.
WHO imesema kuvielewa aina mpya ya virusi vinaweza kuchukua wiki kadhaa na kutahadharisha ya masharti ya kusafiri.