Vyombo vya habari vinasema utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden unapanga kutumia dola bilioni tano kununua kidonge kipya cha majaribio cha Pfizer cha kuzuia COVID-19 kinachotosha kutumika kwa matibabu takriban milioni 10.
Maelezo hayo yanakuja siku moja baada ya kampuni ya kutengeneza dawa Marekani kutangaza kuwa imetia saini mkataba na Medicines Patent Pool yenye makao yake mjini Geneva, kundi la afya ya umma linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuidhinisha watengenezaji dawa mbadala ili kutengeneza kidonge chao cha majaribio cha COVID-19 kwa nchi 95.
Makubaliano hayo yatafanya kidonge hicho kupatikana katika nchi za kipato cha chini na cha kati zinazojumuisha takribani asilimia 53 ya watu duniani.