Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:57

Mataifa yasitisha safari za ndege kutoka Afrika Kusini kufuatia aina mpya ya virusi


FILE - FILE - Mama akidungwa chanjo aina ya Pfizer dhidi ya COVID-19 katika kitongoji cha Diepsloot Johannesburg, Oct. 21, 2021. (AP Photo/Denis Farrell, File)
FILE - FILE - Mama akidungwa chanjo aina ya Pfizer dhidi ya COVID-19 katika kitongoji cha Diepsloot Johannesburg, Oct. 21, 2021. (AP Photo/Denis Farrell, File)

Nchi za Asia na Ulaya zimeweka Ijumaa masharti makali ya usafiri baada ya aina mpya ya virusi vya corona kugunduliwa huko Afrika Kusini.

Wakati huohuo, Umoja wa Ulaya na India zimetangaza masharti makali ya kudhibiti usafiri kwenye mipaka.

Uingereza imepiga marufuku safari za ndege kutoka Afrika kusini na kuomba wasafiri raia wa Uingereza kukaa karantini wakirudi nyumbani kutoka huko. Naye mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema Umoja wa Ulaya pia unalengo la kusitisha safari za ndege katika eneo lake.

Idara ya usalama wa afya ya Uingereza imesema aina hiyo mpya ya virusi ina protini kali ambayo ni tofauti kabisa na ile ambayo ilitumiwa kutengeneza chanjo ya COVID-19.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linafanya mkutano wa wataalamu wa afya leo kujadili aina hiyo mpya ya virusi vya corona na athari zake.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG