Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:40

Baadhi ya raia wa Marekani na Uingereza ni miongoni mwa watu wanaoshikiliwa Ethiopia


Maandamano ya kuunga serikali mkono mjini Addis Ababa, Novemba,7
Maandamano ya kuunga serikali mkono mjini Addis Ababa, Novemba,7

Shirika la habari la AP limesema kwamba raia wa Marekani na Uingereza ni miongoni mwa watu wanaoshikiliwa pamoja na watu wa kabila la Tigrinya, wakati hali ya tahadhari iliyotangazwa na serikali ya Ethiopia ikiendelea.

Maelfu ya watu kutoka kabila la Tigrinya kwenye mji mkuu wa Addis Ababa pamoja na sehemu nyingine za taifa hilo la pili kwa wingi wa watu barani Afrika tayari wamezuiliwa wakati kukiwa na hofu kwamba wengine wengi watakamatwa kwenye msako unaoendelea nchini humo.

Alhamis serikali imeamuru wamiliki wa nyumba za kupanga wapeleke orodha za wapangaji wao kwa polisi. Wakati hayo yakijiri ripoti zimesema kwamba baadhi ya wanaume walionekana wakiwa wamebeba vijiti kwenye barabara, wakati baadhi yao wakiomba watu wa Tigrinya wajitambulishe kwao.

Serikali ya Ethiopia imesema kwamba inafanya msako dhidi ya watu wanaoshukiwa kuunga mkono vikosi vya TPLF ambavyo vinasemekana kuelekea kwenye mji mkuu wa Addis Ababa kufuatia makabiliano ya takriban mwaka mmoja dhidi ya jeshi la Serikali kuu.

Makundi ya haki za binadamu, mawakili pamoja na wanafamilia wamedai kwamba ukamataji unaoendelea dhidi ya watoto na wakongwe unafanyika kwa misingi ya kikabila. Binti ya raia wa Uingereza Meron Kiros ameambia AP kwamba baba yake Kiros Amdermariam Gebreab, ambaye ameishi Uingereza kwa zaidi ya miaka 25, na aliyekuwa ametembea Ethiopia kwa masomo ya shahada ya uzamivu, pia amezuiliwa baada ya kukamatwa wakati akiwa kwake nyumbani kwenye mji mkuu.

Serikali ya Uingereza imeambia AP kwamba imefahamisha serikali ya Ethiopia kuhusiana na suala hilo. Ripoti zinaongeza kwamba huenda kuna raia wawili wa Marekani walioko miongoni mwa watu waliozuiliwa.

XS
SM
MD
LG