Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:04

Marekani: Kura ya kutaka kumuondoa spika Johnson kupigwa wiki ijayo

Mbunge wa chama cha Republican Marjorie Taylor Greene aliyemtaka Spika Johnson kujiuzulu.
Mbunge wa chama cha Republican Marjorie Taylor Greene aliyemtaka Spika Johnson kujiuzulu.

Wabunge wa Marekani watapiga kura wiki ijayo, itakayobaini iwapo Spika wa baraza la wawakilishi Mike Johnson atasalia mamlakani, kwenye mojawapo ya nyadhifa za juu za uongozi katika serikali ya Marekani.

Johnson - ambaye amekuwa spika tangu mwezi Oktoba mwaka jana - anakabiliwa na tishio kutoka ndani ya chama chake. Mbunge wa chama cha Republican Marjorie Taylor Greene alimtaka Johnson kujiuzulu siku ya Jumatano, akisema amesaliti chama kwa kukiuka kanuni zilizofuatwa na rais wa zamani Donald Trump na vuguvugu lake la “Ifanye Marekani kuwa Kuu tena” au kwa kifupi.

Ikiwa hatajiuzulu, Greene anasema ataitisha kura ya kumuondoa.

Juhudi hizo za kiutaratibu, ni za hivi punde zaidi katika nyingine kadhaa zilizibua mtafaruku, za kutaka kumubadilisha spika wa Baraza la Wawakilishi, huku Warepublican wakijaribu kutawala, lakini wakiwa na idadi ndogo ya wajumbe wanaowawezesha kufanya hivyo.

Lakini tofauti na wakati wabunge Wakademocrat waliungana na Warepublican kumwondoa spika aliyemtangulia Johnso, Kevin McCarthy mamlakani mwaka jana, hali haitakuwa hivyo wakati huu.

Kiongozi wa Wademokrat katika baraza la wawakilishi Hakeem Jeffries alitangaza kupitia taarifa Jumanne "Wademokrat watapinga misismamo ya itikadi kali, ya Warepublican.

Forum

XS
SM
MD
LG