Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:26

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa yupo Lebanon kwa juhudi za kidiplomasia


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Stephane Sejourne. March 30, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Stephane Sejourne. March 30, 2024.

Séjourné anatarajiwa kukutana na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon na spika wa bunge la Lebanon.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné amewasili nchini Lebanon leo Jumapili kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kutafuta ufumbuzi kwa mzozo katika mpaka wa Lebanon na Israel.

Séjourné anatarajiwa kukutana na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon na spika wa bunge la Lebanon, mkuu wa jeshi, waziri wa mambo ya nje na waziri mkuu wa muda.

Kundi la wanamgambo wa Lebanon- Hezbollah linapambana karibu kila siku na vikosi vya Israel katika mkoa wa mpakani na wakati mwingine zaidi ya hapo, kwa karibu miezi saba kwa vita vya Israel dhidi ya mshirika wa Hezbollah, Hamas huko Gaza.

Mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watu 350 nchini Lebanon wengi wao wapiganaji wa Hezbollah na makundi washirika lakini pia ikijumuisha raia zaidi ya 50. Mashambulizi yaliyofanywa na Hezbollah yameua raia 10 na wanajeshi 12 nchini Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG