Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:02

Spika wa bunge la Uganda ameekewa vikwazo na Uingereza kutokana na wizi wa mabati


Spika wa bunge la Uganda Anita Among lakiongoza kikao cha bunge, Kampala, Uganda, March 9, 2023.
Spika wa bunge la Uganda Anita Among lakiongoza kikao cha bunge, Kampala, Uganda, March 9, 2023.

Serikali ya Uingereza imetangaza vikwazo kadhaa dhidi ya spika wa bunge la Uganda na maafisa wengine wa ngazi ya juu serikalini.

Spika Anita Among na wabunge wawili wa chama tawala cha NRM, wamewekewa vikwazo vya usafiri kuingia Uingereza na mali zao kuzuiliwa, kutokana na ufisadi.

Wengine ni waliokuwa mawaziri wa eneo la Karamoja Mary Kitutu na Agnes Nandutu.

Walipatikana na maelfu ya mabati ya wizi yaliyokuwa yametolewa na serikali kwa ajili ya kuwajengea nyumba watu wa Karamoja.

Taarifa ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Andrew Mitchell, imesema kwamba maafisa hao walinufaika na mali ya wizi na kwamba ujumbe wa Uingereza ni kwamba watu wanaonufaika na wizi wa raslimali za serikali zinazostahili kuwanufaisha wengine lazima waajibishwe.

Kitutu na Nandutu wamefunguliwa mashtaka ya ufisadi katika mahakama ya Uganda, na kusimamishwa kazi kama mawaziri.

Forum

XS
SM
MD
LG