Kuachia madaraka kwa Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Ujasusi Dan Coats na naibu wake, Sue Gordon, kumekuja wakati mgogoro unaongezeka kati ya China na harakati za waandamanaji Hong Kong na wakati kuna uwezekano wa migogoro mingine kuwa inatokota katika Ghuba ya Uajemi, Rasi ya Korea na kwengineko.
Trump alitangaza kujiuzulu kwa Coats kupitia ujumbe wa Twitter mwezi Julai na baadae chini ya wiki mbili zilizofuatia katika ujumbe wa tweet alieleza kujiuzulu kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuu ya Ujasusi ya Taifa Sue Gordon,ambaye alikuwa ndiye anatarajiwa kuwa kaimu mkurugenzi.
Lakini katika ujumbe uliyokuwa umeambatanishwa na barua ya kujiuzulu, Gordon aliweka wazi kuwa kuacha kwake kazi kulikuwa ni kitendo cha heshima na uzalendo lakini siyo kipaumbele chake.” “Utengeneze timu yako,” alieleza.
Trump alimchagua Coats, mbunge wa zamani wa chama cha Republikan na aliyewahi wakati mmoja kuwa balozi wa Marekani Ujerumani, kuwa afisa wake wa ujasusi wa ngazi ya juu mara tu baada ya kuchukua madaraka ya urais.
Coats alipongezwa na wabunge na wastaafu wa jumuiya ya majasusi ya Marekani kwa “kuwakosoa walioko madarakani,” na tathmini yake kwa umma mara kwa mara ilikinzana na matamko ya rais.