“Russia imeendeleza uchokozi, fursa walioichukua kutokana na kuwepo sera dhaifu dhidi ya uchokozi huo. Hiyo ni mwisho sasa,” Pompeo ataiambia kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti, kwa mujibu wa nukuu za ushuhuda wake.
Korea Kaskazini na Iran zinategemewa kuwa ni sehemu ya mazungumzo hayo Alhamisi.
Kutofautiana kati ya Rais Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Rex Tillerson kulipelekea kufukuzwa kwa waziri huyo mwezi Machi.
Lakini Stephen Pompeo wa Kikundi cha Kukabiliana na Migogoro ya Kimataifa anasema iwapo atathibitishwa, Pompeo hatokabiliwa na vipingamizi alivyovikabili Tillerson.