Shirika la habari la Sudan-SUNA liliripoti kwamba Rais wa Sudan Omar al-Bashir amemuondoa madarakani mkuu wake wa usalama na kumrudisha ofisa mwandamizi ambaye alisaidia kuanzisha mashauriano ya usalama na Marekani baada ya mashambulizi ya Septemba 11 yaliyotokea mjini Washington na New York nchini Marekani.
Shirika hilo lilisema Salah Abdallah Mohamed pia anajulikana kama Salah Gosh ambaye alihudumu kama mkuu wa idara ya ujasusi na idara za usalama wa nchi-NISS kati ya mwaka 2004 na 2009 alirudishwa tena kwenye wadhifa huo akichukua nafasi ya Mohammed Atta al-Moula ambaye alihudumu nafasi hiyo tangu mwaka 2009.
Uhusiano kati ya Sudan na Marekani umeimarika chini ya utawala wa Rais Donald Trump ambaye mwaka uliopita aliondoka vikwazo vya muda mrefu dhidi ya Sudan akisema nchi hiyo ilipiga hatua kupambana na ugaidi na kusitisha mahangaiko ya kibinadamu. Hii ni hatua kubwa kufikiwa kwa serikali ya Bashir.
Lakini Marekani iliendelea kuiweka Sudan kwenye orodha ya Marekani ya mataifa yanayofadhili uhaidi ikiwa pamoja na Iran na Syria ambazo zimewekewa marufuku yasilaha na vizingiti katika kupata msaada wa Marekani kulingana na maafisa wa Marekani.