Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:42

Mafuriko : Viwango vya maji bado viko juu katika miji mingi Ujerumani


Watu wakisafisha nyumba zao kutokana na mafuriko huko Bad Neuenahr-Ahrweiler, Ujerumani, Jumamosi, Julai 17, 2021. (AP Photo/Michael Probst)
Watu wakisafisha nyumba zao kutokana na mafuriko huko Bad Neuenahr-Ahrweiler, Ujerumani, Jumamosi, Julai 17, 2021. (AP Photo/Michael Probst)

Wafanyakazi wa uokoaji wanaendelea na zoezi la kuwatafuta manusura katika sehemu zilizoharibiwa na mafuriko huko magharibi mwa Ujerumani Jumamosi, wakati viwango vya maji bado vipo juu katika miji mingi.

Wakati huohuo vyanzo vya habari nchini Ujerumani vinaendelea kuripoti kuwa nyumba zinaendelea kuanguka katika janga baya la kiasili kutokea nchini humo kwa muda wa nusu karne.

Watu 133 wamekufa kwenye mafuriko hayo, wakiwemo watu 90 katika wilaya ya Ahrweiler, kusini mwa Cologne, kulingana na makadirio ya polisi ya leo Jumamosi.

Taarifa zinaeleza kuwa bado mamia ya watu hawajapatikana.

Wakaazi 700 walihamishwa Ijumaa jioni, baada ya bwawa kupasuka katika mji wa Wassenberg, karibu na Cologne, maafisa walisema.

Kwa siku kadhaa zilizopita mafuriko, ambayo yameathiri zaidi majimbo ya Rhineland Palatinate na North Rhine-Westphalia, yamesababisha jamii nzima kukosa umeme na mawasiliano.

Mafuriko hayo pia, yameathiri maeneo ya Ubelgiji na Uholanzi. Watu 20 wamekufa nchini Ubelgiji.

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier na Armin Laschet, Waziri mkuu wa jimbo la North Rhine-Westphalia, walitarajiwa leo kutembelea Erftstadt, moja ya miji iliyoathiriwa sana na mafuriko.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali.

XS
SM
MD
LG