Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:42

Polisi wa Ujerumani wanatafuta chanzo cha shambulizi la kisu lililosababisha vifo


Polisi wa Ujerumani wakielekea eneo la tukio katika mji wa Wuerzburg
Polisi wa Ujerumani wakielekea eneo la tukio katika mji wa Wuerzburg

Mshukiwa katika tukio ana umri wa miaka 24 ni raia wa Somalia ambaye alipigwa risasi na polisi wa Ujerumani na alikamatwa baada ya shambulizi la Ijumaa inaripotiwa alikuwa anajulikana na polisi na alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa wa akili siku chache kabla ya uhalifu huo

Wachunguzi nchini Ujerumani wanatafuta chanzo kilichopelekea shambulizi katika mji wa Wuerzburg nchini humo ambapo mtu mmoja aliyekuwa na kisu aliwaua watu watatu na kuwajeruhi wengine wapatao watano.

Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24 ni raia wa Somalia ambaye alipigwa risasi na polisi wa Ujerumani na alikamatwa baada ya shambulizi la Ijumaa lililotokea katika eneo la katikati mwa jiji. Polisi walisema maisha ya mshukiwa hayakuwa hatarini.

Afisa mkuu wa usalama wa Bavaria, Joachim Herrmann, alisema mshukiwa huyo alikuwa anajulikana na polisi na alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa wa akili siku chache kabla ya tukio. Alisema hiyo Ijumaa kwamba mshukiwa hakuelezea msimamo mkali wa kiislam ulichangia hilo kwa sababu shahidi mmoja aliripoti akisikia mshukiwa akisema kwa sauti kubwa “Allahu Akbar” maneno ambayo kwa lugha ya kiarabu inamaanisha “Mungu ni mkubwa”.

XS
SM
MD
LG