Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 08, 2025 Local time: 18:41

Libya yatangaza sitisho la mapigano


Wakimbizi wakisubiri kuvuka mpaka wa Libya na kuingia Ras Ajdir nchini Tunisia.
Wakimbizi wakisubiri kuvuka mpaka wa Libya na kuingia Ras Ajdir nchini Tunisia.

Kiongozi wa Libya ametangaza sitisho la mapigano na yuko tayari kwa mazungumzo.

Libya imetangaza sitisho la mapigano na kusema iko tayari kuanzisha mjadala na upande wa upinzani. Serikali ilitoa tangazo hilo hivi leo, siku moja baada ya baraza la usalama la Umoja Mataifa kupitisha azimio ambalo linapiga marufuku usafiri wa ndege nchini humo.

Mataifa yenye nguvu duniani yatalifikiria tangazo la Libya la sitisho la mapigano katika kikao cha dharura kitakachofanyika Paris Jumamosi. Wajumbe wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Umoja wa Ulaya na Marekani wamesema watahudhuria mkutano huo.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Profesa Xavery Lwaitama wa chuo kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania anasema, baraza la usalama limechukua muda mrefu kumchukulia hatua kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi.

"Wapinzani wa Gadhafi na wananchi wa kawaida wameathiriwa na wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo. Ilikuwa ni wajibu wa baraza la usalama kuchukua mwanzoni tu pale ilipobainika kuwa serikali ya Libya imepania kuwatokomeza wapinzani."

Naye afisa wa habari wa shirika la kimatiafa la uhamiaji - IOM -, Jumbe Omar Jumbe anasema idadi ya walibya wanaokimbia mapigano imepungua katika wiki za karibuni, lakini shirika lake bado linahitaji msaada wa fedha ili kuwahudumia wakimbizi ambao tayari wako katika kambi yao.

XS
SM
MD
LG