Wanajeshi wa serikali ya kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi waliwafurusha wapiganaji wa upinzani kutoka mji huo muhimu wa mafuta baada ya kuchukua tena udhibiti wake siku ya Jumatano.
Ripoti za vyombo vya habari kutoka Ras Lanuf zinaeleza kwamba, wapiganaji walikuwa wanarudi nyuma kufuatia mapigano makali ya roketi.
Ripoti zinaeleza idadi kubwa ya wapiganaji walikimbia wakitumia malori madogo na hivyo kupoteza tena udhibiti wa maeneo walokombowa tangu mwishoni mwa wiki walipokuwa wanaelekea upande wa magharibi.
Hali katika uwanja wa mapigano ilianza kubadilika Jumanne usiku pale wanajeshi wa Libya walipoanza kuwashambulia wapiganaji kwa mizinga na roketi na kusababisha hofu kubwa katika mji wa Ras Lanuf.