Makombora na mizinga ya kushambulia ndege zimekuwa zikifyetuliwa kwenye anga ya mji mkuu wa Libya Tripoli kukiwepo na mlipuko mmoja uliotingisha mji mkuu huo wakati mataifa zaidi ya maghariri yanajiunga na ushirika wa kutekeleza marufuku ya Umoja wa Mataifa ya kutorusha ndege juu ya anga ya Libya.
Sauti za makombora hayo na milipuko ilisikika huko Tripoli mara tu baada ya usiku kuingia siku ya Jumatatu. Televisheni ya taifa ya Libya ilisema mji mkuu huo unashambuliwa tena na ndege za vita za mataifa ya ushirika.
Mapema Jumatatu, mkuu wa kitengo cha Afrikja cha jeshi la Marekani alisema ndege hizo ushirika zinafanya doria zaidi katika anga la Libya nyakati za mchana huku kukiwa na mataifa saba yanayoshiriki pamoja na Marekani.
Akizungumza katika makao yake makuu yaliyoko Ujerumani Generali Carter Ham alisema mataifa mengine ikiwemo Ubelgiji, uingereza, Canada, Denmark, Ufaransa na Hispania. Alisema lengo la mashmabulio ya anga ni kuwalinda raia wa Libya na hivi sasa kuhakikisha hakuna ndege za Libya zinaruka huko mashariki na magharibi ya nchi.
Wakati huo huo jeshi la Marekani limethibitisha kuanguka kwa ndege yake huko Libya na kwamba marubani wawili wa ndege hiyo ya aina F -15 wamepatikana wakiwa salama.