Milipuko mikubwa iliendelea kusikika Alhamisi huko mashariki ya mji mkuu wa Libya Tripoli, wakati operesheni iliyoidhinishwa na Umoja wa Matiafa ya kuzuiya safari za ndege katika anga ya Libya ikingia siku yake ya sita.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa uUaransa Alain Juppe alisema mashambulizi ya anga ya ushirika yanalengo la kulinda raia na yanalenga tu vituo vya kijeshi.
Siku ya Jumatano majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi yalianza tena mashambulizi yake katika mji wa tatu kwa ukubwa huko Libya, Misrata baada ya ndege za magharibi kusitisha kwa muda mashambulizi ya majeshi ya serikali kwa kuyashmabulia kwa mfululizo wa makombora.
Daktari mmoja huko Misrata alisema majeshi yanayomuunga mkono Gadhafi yalifyetua mizinga kiholela ikiwa pia karibu na hospitali pekee kwenye mji huo na pia walenga shababi walifyatulia risasi raia kutoka kwenye mapaa ya majengo.
Hata hivyo waziri mdogo wa mambo ya nje wa Libya Khalid Karim alisistiza Alhamisi kwamba hakukuwa na operesheni zozote za jeshi la ardhini huko Misrata. Majeshi hayao yanayomtii kiongozi wa Libya pia yaliendelea na mashambulizi yake Jumatano katika miji inayoshikiliwa na waasi ya Zinat na Ajdabiya.