Wanadiplomasia wa jopo la nchi za Magharibi na Mashariki ya Kati wamekutana mjini Doha, Qatar na kukubaliana juu ya utaratibu wa muda wa kutowa fedha kuwasaidia wapinzani kupata fedha kwa matumizi ya harakati zaoo.
Wanadiplomasia kutoka Ufaransa, Uingereza, Marekani, Umoja wa Mataifa, Umoja wa nchi za Kiarabu na Umoja wa Afrika walihudhuria mkutano wa Doha ili kuanda mpango wa kuratibu juhudi za kimataifa katika kukabiliana na mzozo wa Libya.
Katika taarifa yao ya mwisho, jopo limetowa wito kwa kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi kuacha madaraka, likisema yeye na serikali yake wamepoteza haki zote za kutawala.
Mwanamfalme wa Qatar amesema jumuia ya kimataifa ina muda mdogo sana kujipanga na kuwapatia wapiganaji vifaa vinavyo hitajika kupigana.
Jumatano usiku rais Nicolas Sarkozy na waziri mkuu wa UIngereza David Cameron walikuwa na mazungumzo mjini Paris juu ya mzozo wa Libya.
Afisis ya Bw. Cameron imeeleza kwamba viongozi hao wawili walijadili juu ya namna ya kuongeza shinikizo la kijeshi dhidi ya Libya.