Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 09, 2025 Local time: 11:21

Marekani na majeshi ya Ushirika yashambulia Libya


Kombora la Tomahawk likifyetuliwa kutoka manuwari ya Marekani ya USS Barry kutoka bahari ya Mediterranean.
Kombora la Tomahawk likifyetuliwa kutoka manuwari ya Marekani ya USS Barry kutoka bahari ya Mediterranean.

Majeshi ya ushirika wa magharibi yakiongozwa na Marekani yamefanya mashambulio ya makombora dhidi ya vituo muhimu vya kijeshi nchini Libya.

Majeshi hayo yamefyetua zaidi ya makombora 100 ya aina ya Tomahawk dhidi ya vituo muhimu vya ulinzi katika sehemu mbali mbali za Libya kama sehamu ya operesheni ya kuwalinda wananchi kutoka majeshi ya kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi.

Naibu Admirali wa Marekani William Gortney aliefafanua Jumamosi juu ya mashambulio hayo yaliyopewa jina la "Operation Odyssey Dawn", masaa machache baada ya makombora kuanza kushambulia zaidi ya vituo 20 vya jeshi la Libya.

Amesema, "jeshi la Marekani limeanza na litaendelea kutumia uwezo wake wa kipekee kubuni hali ambayo sisi na washirika wenzetu tutaweza kutekeleza kwa kikamilifu azimio la Umoja wa Mataifa. Kazi yetu hivi sasa ni kutayarisha uwanja wa mapambano kwa namna ya kuwaruhusu washirika wetu kuongoza katika utekelezaji."

Alisema Admirali Sam Locklear anaongoza operesheni hiyo kutokea manwari ya USS Mount Whitney iliyoko katika bahari ya Mediterranean.

Siku ya Alhamisi Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa liliidhinisha azimo la kuruhusu vikosi vya kigeni kutumia nguvu za kijeshi kuwalinda wananchi wa Libya na kutekeleza amri ya kutoruhusu usafiri wa ndege juu ya anga ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG