Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 09, 2025 Local time: 21:23

Arab League yajadili mzozo wa Libya


Wapiganaji waasi huko Libya wanajiepusha na makombora yanayolipuka wakati wa mapambano na majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi, kilometa chache nje ya mji wa unaozalisha mafuta wa Ras Lanuf.
Wapiganaji waasi huko Libya wanajiepusha na makombora yanayolipuka wakati wa mapambano na majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi, kilometa chache nje ya mji wa unaozalisha mafuta wa Ras Lanuf.

Kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi azidishiwa shinikizo kuacha kuwashambulia wapinzani wake.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu wanakutana nchini Misri hivi leo Jumamosi kujadili uwezekano wa kuweka marufuku ya kurusha ndege huko Libya ili kuzidisha shinikizo kwa kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi ili kumaliza ghasia dhidi ya waasi.

Maafisa wa juu wa Jumuiya ya nchi za kiarabu, Arab League, wanasema wawakilishi kutoka Tripoli wataenguliwa katika mikutano hiyo, wakati ambapo majeshi ya Bwana Gadhafi yamezidisha mashambulizi yake kwa majeshi ya upinzani.

Rais wa Marekani, Barack Obama amesema jana kuwa hajaondoa mezani njia zozote kuhusu uwezekano wa majibu kwa ukamataji unaofanywa na Bwana Gadhafi dhidi ya wapinzani wa serikali.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walikutana Brussels jana Ijumaa na kukubaliana kwamba upinzani wa National Council huko Libya ni taasisi halali ya kisiasa. Hata hivyo, mataifa 27 wanachama wa umoja huo wamesita kulitambua moja kwa moja baraza hilo kama ilivyofanya Ufaransa.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu inasema Libya imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Umoja Mataifa inasema mzozo huo umesababisha zaidi ya vifo elfu moja na kuwalazimisha takriban watu laki mbili na nusu kukimbia nchi.

Wakati huo huo, kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa, Total imesema jana kuwa mzozo unaoendelea huko Libya umesababisha wapunguze uzalishaji mafuta. Mtendaji mkuu wa kampuni ya Total, Christophe de Margerie amesema kuwa uzalishaji wa mapipa milioni moja nukta sita kwa siku hivi sasa umeshuka hadi mapipa laki mbili na laki tatu kwa siku.

XS
SM
MD
LG