Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 02:54

Kremlin yasema vita vya Ukraine vitaendelea


Russia Ukraine War
Russia Ukraine War

Russia imesema kwamba vita vyake nchini Ukraine vitaendelea hadi malengo yake yaliyowekwa na rais Vladimir Putin yamefikiwa,  iwe kwa njia ya kijeshi au mashauriano.

Putin anataka Ukraine kuacha utashi wake wa kujiunga na muungano wa ulinzi wa NATO na kuondaa wanajeshi wake kutoka mikoa minne ambayo Russia inadai ni yake.

Ukraine imeyakataa masharti hayo ikisema ni sawa na kujisalimisha.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kuwa operesheni maalum ya kijeshi itamalizika pale malengo yote yaliyowekwa na rais Putin yamefanikiwa.

Peskov amesema hakuna mazungumzo yanafanyika kwa sasa kati ya Moscow na Kyiv kwa sababu Ukraine imekataa aina yoyote ya mashauriano.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alisema jana jumatatu kwamba kuna haja ya kufanyika juhudi za kidiplomasia ili kumaliza vita hivyo, na kuzungumzia swala la kupelekwa kwa wanajeshi wa nje nchini Ukraine hadi nchi hiyo itakapojiunga na NATO.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Ukraine Septemba 20, 2023. Picha na ANGELA WEISS / AFP
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Ukraine Septemba 20, 2023. Picha na ANGELA WEISS / AFP

Forum

XS
SM
MD
LG