Russia imejumuisha maeneo ambayo imechukuwa huko Ukraine katika ripoti yake ya hivi karibuni ya makadirio ya utoaji wa hewa chafu kwenye Umoja wa Mataifa, ikipelekea kupingwa na maafisa wa Ukraine na wanaharakati katika mkutano wa hali ya hewa wa COP29 wiki hii. Hatua hiyo ya Moscow inakuja wakati Rais wa Russia Vladimir Putin
Anaelekeza mawazo yake katika uwezekano wa mazungumzo ya makubaliano ya amani na rais anayeingia madarakani wa Marekani
Donald Trump ambaye anaweza kuamua hatima ya maeneo hayo makubwa ya ardhi.
Tunaona kuwa Russia inatumia majukwaa ya kimataifa
kuhalalisha matendo yao, kuhalalisha kuchukua maeneo, Naibu Waziri wa Mazingira wa Ukraine Olga Yukhymchuk aliiambia Reuters.
RUSSIA UKLRAINE COP 29
Forum