Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:36

Kim Jong Un aishutumu Marekani kuongeza mivutano


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipotembelea Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Taifa huko Pyongyang. Picha na KCNA via REUTERS
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipotembelea Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Taifa huko Pyongyang. Picha na KCNA via REUTERS

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameishutumu Marekani kwa kuongeza mvutano na uchokozi, amesema rasi ya Korea haijawahi kukabiliwa na hatari ya vita vya nyuklia kama sasa, shirika la KRT linalomilikiwa na serikali limesema.

Katika hotuba yake kwenye maonyesho ya kijeshi siku ya Alhamis mjini Pyongyang, Kim alisema uzoefu wake wa awali wa mashauriano na Washington ni kuangazia sera yake ya “uchokozi na uadui” dhidi ya Pyongyang, KRT imesema.

Wakati wa utawala wa Rais-mteule Donald Trump, Trump na Kim walifanya mikutano mitatu isiyo ya kawaida huko Singapore, Hanoi,na mpakani mwa Korea mwaka 2018 na 2019, imeshindwa kufanikisha matokeo yoyote Madhubuti.

Kim katika hotuba yake ametaka kuendeleza na kuboresha silaha kuwa za “kisasa zaidi” na kuapa kuendelea kuboresha uwezo wa ulinzi na kuimarisha nafasi ya kimkakati ya nchi hiyo, KRT imesema.

Hotuba ya hivi karibuni ya Kim, imekuja kufuatia ukosoaji wa kimataifa kuhusu ongezeko la ushirikiano wa kijeshi kati ya Pyongyang na Moscow, wakati Korea Kaskazini ikiwa imetuma zaidi ya wanajeshi 10,000 kwenda Russia kuisaidia katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG