Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:59

Korea kaskazini imevuruga GPS ya Korea Kusini


Mitabo ya GPS inayoonekana kuvurugwa na Korea kaskazini.
Mitabo ya GPS inayoonekana kuvurugwa na Korea kaskazini.

Korea kaskazini imechakachua mtambo wa GPS kwa maksudi jana ijumaa na leo jumamosi, katika oparesheni ambayo imeathiri safari kadhaa za meli na darzeni za ndege za abiria nchini Korea kusini.

Hayo ni kulingana na jeshi la Korea kusini.

Madai hayo yanajiri wiki moja baada ya Korea kaskazini kufanyia majaribio kile ilisema kuwa ni kombora lenye nguvu sana aina ya ICBM, ikiwa ni jaribio la kwanza tangu nchi hiyo iliposhutumiwa kupeleka wanajeshi wake kuisaidia Russia kupigana nchini Ukraine.

Korea kusini ilifyatua kombora lake la masafa marefu kuelekea baharini jana Ijumaa katika hatua ya kuonyesha nguvu za kujibu uchokozi wa Korea kaskazini

Uhusiano kati ya Korea kusini na Kaskazini umeharibika sana katika miaka ya hivi karibuni, Korea kaskazini ilifyatua makombora kadhaa ya masafa marefu ikikiuka vikwazo vya umoja wa mataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG