Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:00

Beijing yatakiwa kuizuia Korea Kaskazini kupeleka vikosi Russia


Washirika kadhaa wa kibiashara wa Beijing, wanamsihi rais wa China, Xi Jinping, kutoa msukumo zaidi kwa Korea Kaskazini, ili iachane na mpango wa kupeleka wanajeshi wake Russia.

Zaidi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini 10,000 wamekwenda katika uwanja wa mapambano katika vita dhidi ya Ukraine.

Mwito huo imesisitizwa katika mikutano miwili mikubwa ya juma hili ya Brazil, na Peru, ambao uligusia hali ya kushangaza ambapo kiongozi wa China, anajikuta katika wasaa mgumu wa kuweka mambo sawa baina ya Russia na mataifa ya magharibi.

Katika mkutano wa pamoja na wanahabari, mjini Brasilia, Alhamisi, na Rais wa Brazil, Luis Inacio Lula da Silva, Rais Xi, ametoa mwito kwa uwepo wa sauti zaidi zinazotaka amani nchini Ukraine.

Amerejea ujumbe wa Mei wa Brazil na China, unaotaka uwepo wa mazungumzo ya kumaliza mgogoro kwa suluhisho la kisiasa.

Forum

XS
SM
MD
LG