Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:34

Kiongozi wa Hong Kong aeleza msimamo wa serikali


Wanafunzi wanaosomea udaktari wakionesha mshikamano wakati wa maandamano dhidi ya vitendo vya ukatili vilivyofanywa na polisi katika Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Hong Kong, Septemba 5, 2019. REUTERS/Anushree Fadnavis - RC195077EF30
Wanafunzi wanaosomea udaktari wakionesha mshikamano wakati wa maandamano dhidi ya vitendo vya ukatili vilivyofanywa na polisi katika Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Hong Kong, Septemba 5, 2019. REUTERS/Anushree Fadnavis - RC195077EF30

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amesema anafahamu na kuheshimu na kuunga mkono hatua ya serikali yake kuondoa rasmi muswada wa kuwapeleka watuhumiwa China bara ikiwa ni hatua ambayo anatumaini itasaidia mji huo hatimaye kuondokana na maandamano na ghasia. 

“Uamuzi huu ni moja ya maamuzi ya serikali ya Hong Kong .Kama ambavyo muswaada huo ulitangazwa, ulipenedekezwa na kuchukuliwa na serikali.

Lakini nina hakika mnataka kuuliza msimamo wa serikali kuu. Kwa hiyo niongeze kusema kwamba wakati wote wa mchakato huu serikali kuu ilichukuwa msimamo ulioeleweka kwao kwa nini tunaamua kufanya hivi. “

Katika mkutano na waandishi wa habari Lam aliulizwa mara kadhaa kwa nini imemchukua muda mrefu kuchukua hatua hiyo ya kuondoa muswada huo licha ya ghasia mbaya kuongezeka, lakini alikwepa kujibu maswali hayo.

Ameondoa muswaada huo ambao uliingiza eneo hilo lililo chini ya udhibiti wa China katika mzozo mbaya zaidi kuliko wowote katika miaka kadhaa.

Jumatano soko la fedha la Hong Kong –HSI liliongezeka kwa zaidi ya asilimia 4 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya tangazo. Na alhamisi soko liliongezeka kwa asilimia 0.4 ilipofika mchana.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG