Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:19

Hong Kong : Vyama vya wafanyakazi vyapinga ufukuzaji kazi holela wa shirika la ndege


Askari akielekeza silaha ya moto kwa wanandamanaji Hong Kong, Jumapili, Agosti 25, 2019.
Askari akielekeza silaha ya moto kwa wanandamanaji Hong Kong, Jumapili, Agosti 25, 2019.

Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi Hong Kong wameandamana Jumatano dhidi ya shirika la ndege la mji huo, Cathay Pacific kwa kuwafukuza kazi wafanyakazi wake kwa madai ya kuwa wanamafungamano na maandamano yanayoshinikiza kuwepo demokrasia yanayoendelea kipindi hiki cha joto..

Shirika la habari la AP limeripoti kuwa bango nyuma ya jukwaa katika bustani ya umma iliyoko katikati ya mji lilisomeka kama “Sitisheni ufukuzaji kazi” na “Acheni kuwatishia wafanyakazi wa CX,” wakikusudia shirika hilo la ndege.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi Hong Kong wamesema kuwa wafanyakazi 20 wamefukuzwa kazi au wamelazimishwa kujiuzulu, wakiwemo marubani, wahudumu wa ndege na mameneja. Mkurugenzi mtendaji mkuu Rupert Hogg alijiuzulu mapema Agosti akiwajibika baada ya matukio hayo, shirika hilo la ndege lilisema.

Cathay amethibitisha kufukuzwa kwa wafanyakazi kadhaa katika kipindi cha wiki mbili. Imesema kutokana na sababu mbalimbali, kama vile rubani mmoja aliyetumia vibaya taarifa za kampuni au mwengine anayekabiliwa na kesi, bila ya kutaja maandamano. Cathay ambaye ni rubani alishtakiwa kwa kufanya vurugu wakati wa maandamano.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi wameita maandamano kwa jina la Cathay Dragon, kundi la Cathay la shirika la ndege, aliyemfukuza mkuu wa chama cha wafanyakazi wahudumu wa ndege.

Mamlaka ya usafiri wa anga China wamemshinikiza Cathay kuwapiga marufuku wafanyakazi wanaofanya kazi katika ndege za bara iwapo wataunga mkono “maandamano haramu.” Serikali kuu ya China imekuwa ikipinga maandamano yanayofanyika Hong Kong ambayo inautawala wake wakujitegemea.

XS
SM
MD
LG