Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:02

China yapeleka vikosi vipya Hong Kong


Waandamanaji wakiwa wamezungukwa na moshi wa mabomu ya kutoa machozi huko Tsuen Wan, katika Jiji la Hong Kong, Agosti. 25, 2019.
Waandamanaji wakiwa wamezungukwa na moshi wa mabomu ya kutoa machozi huko Tsuen Wan, katika Jiji la Hong Kong, Agosti. 25, 2019.

China imepeleka vikosi vipya katika kituo chake cha kijeshi Hong Kong katikati ya mgogoro wa kisiasa uliyokuwa mbaya zaidi tangu Hong Kong kurejea katika utawala wa China mwaka 1997.

Shirika la habari la serikali, Xinhua, limeeleza Alhamisi kupelekwa kwa vikosi hivyo ni utaratibu wa kawaida wa kubadilisha wanajeshi na vifaa katika kambi ya jeshi la ukombozi wa wananchi kwenye jiji hilo ambalo ni kituo kikuu cha kibiashara.

Televisheni ya taifa ilionyesha picha za video za magari yasiyopenya risasi na malori ya kubebea wanajeshi yakiingia katika kambi hiyo baada ya kuvuka mpaka wa mji jirani wa Shenzhen.

Hong Kong imekumbwa kwa takriban miezi mitatu ya mvutano na vurugu za maandamano ambayo yalianza kama ni maandamano dhidi ya muswada wenye utata wa kuwarudisha wahalifu China bara, lakini tangu wakati huo yamebadilika na kushinikiza kuwepo kwa demokrasia zaidi na uchunguzi wa kujitegemea kuangalia madai ya ukatili wa polisi.

Jeshi la polisi la jiji hilo Alhamisi walikataa kutoa kibali kwa kikundi cha wanaharakati cha Civil Human Rights Front kufanya maandamano mengine Jumamosi, ikisema hii ni kwa sababu ya kuhofia kutokea vurugu kati ya polisi na waandamanaji kama ilivyokuwa wakati wa maandamano ya wikiendi iliyopita.

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji maalum dhidi ya waandamanaji ambao walijitenga na kundi kubwa lililokuwa linaandamana kwa amani.

Baadhi ya waandamanaji hao waliwatupia polisi matofali, waliwashambulia kwa fimbo, nondo na kutupa sabuni mitaani ili kufanya polisi wasiweze kupita katika barabara hizo kutokana na utelezi.


Maandamano yaliyopangwa Siku ya Jumamosi yatakuwa ni kilele cha miaka mitano tangu Beijing kukataa Hong Kong kuchagua viongozi wake kidemokrasia.

Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wanahofia kuwa China inaendelea kukandamiza uhuru wa msingi ambao wamekuwa wakinufaika nao tangu mwaka 1997, wakati Hong Kong ilipokabidhiwa kutoka katika utawala wa Uingereza.

XS
SM
MD
LG