Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 11:03

Kenya yaunganishwa na mkonga wa kampuni ya mawasiliano ya Huawei


FILE - Kijana akitumia internet katika mgahawa wa intaneti June 20, 2012 katika eneo la Kibera Nairobi. AFP PHOTO/Tony KARUMBA / AFP PHOTO / TONY KARUMBA
FILE - Kijana akitumia internet katika mgahawa wa intaneti June 20, 2012 katika eneo la Kibera Nairobi. AFP PHOTO/Tony KARUMBA / AFP PHOTO / TONY KARUMBA

China imeunganisha nyaya zenye urefu wa kilomita 15,000 chini ya bahari, za mawasiliano yenye kasi ya juu ya mamilioni ya dola huko nchini Kenya, wakati Beijing ikisonga mbele na kile kilichoelezewa kama “barabara ya hariri ya kidigitali,” ... kwa ajili ya kuboresha mawasiliano ya intaneti.

China imeunganisha nyaya zenye urefu wa kilomita 15,000 chini ya bahari, za mawasiliano yenye kasi ya juu ya mamilioni ya dola huko nchini Kenya, wakati Beijing ikisonga mbele na kile kilichoelezewa kama “barabara ya hariri ya kidigitali,” na Afrika inahitaji miundo mbinu hiyo kwa ajili ya kuboresha mawasiliano ya intaneti.

Kampuni kubwa ya China, Huawei ni wana hisa katika mawasiliano hayo yenye thamani ya dola milioni 425 unaojulikana kama mkonga wa PEACE ambao kirefu chake ni “Pakistan na Afrika Mashariki na Ulaya.” Unatambaa kutoka Asia hadi Afrika na halafu unaingia Ufaransa, ambako unakomea..

Umefika pwani katika mji wa Mombasa Jumanne, huku Mtendaji Mkuu wa kampuni shirika ya eneo Telekom Kenya, Mugo Kibati, amesema mkonga huo utasaidia kukabiliana na kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za intanet katika bara hilo ambalo matumizi ya intanet yako nyuma ukilinganisha na maeneo mengine duniani, lakini ambako idadi ya vijana na mahitaji ya kidijitali yanaongezeka.

“Huu mkonga wenye uwezo wa kiwango cha juu utaisaidia Kenya na eneo hilo katika kukidhi mahitaji ya hivi sasa na siku za usoni ya uwezo wa broadband, itaondoa upungufu wa huduma, itapunguza muda wa kusubiri wakati tunaunganisha mawasiliano na Asia na Ulaya, pia kuwasaidia wanaotoa huduma za mawasiliano zinazoweza kuwa nafuu wka wakenya,” alisema Kibati.

Maendeleo ya Kibiashara

Kwa upande wake, Mkuu wa Operesheni wa Mkonga wa PEACE, Sun Xiaohua, amesema katika taarifa kuwa miundo mbinu hii mipya “italeta maendeleo ya biashara zaidi katika eneo hili.” Kutoka Kenya, mkonga huu baadae utatambaa zaidi kwenda upande wa chini wa pwani ya mashariki ya bara hili hadi Afrika Kusini.

Inakadiriwa kuwa asilimia 95 ya takwimu za kimataifa zinapitia katika mikonga iliyoko chini ya bahari, na kwa upande wa Afrika, China inaongoza, ikiwa na miradi mingi zaidi iliyolenga kuliunganisha bara hilo. Mbali na hiyo ya mkonga wa PEACE, China imependekeza mkonga wa 2Africa ambao utakuja kuwa moja ya miradi mikubwa sana ya chini ya bahari duniani wakati itakapoanza kutumika rasmi mwaka 2024.

Lakini uwekezaji mkubwa wa miundo mbinu ya kidijitali ya China barani Afrika na kwengineko haujafanyika bila ya mivutano, na Washington imeelezea wasiwasi wake wa kina kuwa Beijing inafanya jaribio la kuhodhi mitandao na pia uwezekano upo wa kuitumia kwa ujasusi.

Wasiwasi juu ya usalama

Baadhi ya wachambuzi wana wasiwasi kuwa teknolojia hiyo inaweza kutumika vibaya na viongozi wa kiimla katika bara hilo, lakini Cobus van Staden, mtafiti mwandamizi wa China na Afrika katika Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Afrika Kusini alisema Waafrika walio wengi wanataka mawasiliano bora ya intanet.

“Nafikiri PEACE Cable kwa jumla inaleta matokeo chanya Afrika. Bila s haka, Marekani imeeleza … wasiwasi juu ya hili, hususan kuhusiana na usalama, lakini nafikiri kwa nchi nyingi za Afrika, suala la usalama linatafutiwa uwiano na suala la ukosefu wa mawasiliano,” van Staden aliiambia VOA.

Huawei iliwekewa vikwazo na Marekani wakati wa uongozi wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, lakini kampuni imejenga kiasi cha asilimia 70 ya mitandao ya 4G iliyoko Afrika, na van Staden alisema inaonekana China inashinda katika kinyang’anyiro cha mbio za nguvu za kidijitali barani humo.

“Nafikiri kuna fursa ya ushindani huko, lakini washirika wa magharibi itabidi waongeze bidi,” alisema.

XS
SM
MD
LG