Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:53

China yasema kisanduku cheusi cha ndege ya abiria kimepatikana


Wafanyakazi wa uokoaji wapata kisanduku cheusi katika ajali ya ndege iliyotokea China.
Wafanyakazi wa uokoaji wapata kisanduku cheusi katika ajali ya ndege iliyotokea China.

Mojawapo ya kijisanduku cheusi cha ndege ya abiria iliyoanguka kusini mwa China kimepatikana Jumatano.

Hatua hiyo ni muhimu sana katika uchunguzi wa kubaini kilichosababisha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea China kwa miaka mingi.

Ndege ya shirika la China Eastern, namba MU5735, iliyokuwa imebeba abiria 123 na wafanyakazi wake 9 ilianguka katika sehemu ya milima jimbo la Tengxian, Guangxi.

Ndege hiyo ilikuwa inatoka Kunming na hadi sasa hakuna manusura.

Kupatikana kwa vijisanduku hivyo viwili vya Boeing 737-800 vyenye ujumbe muhimu wa safari za ndege hiyo ni hatua muhimu katika uchunguzi unaoendelea kuhusu ajali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Wuzhou, mkurugenzi wa kituo cha kuchunguza ajali za ndege nchini China Mao Yanfeng, amethibitisha kupatikana kwa vijisanduku hivyo.

Amesema kwamba vijisanduku hivyo vimeharibika sana lakini wachunguzi wanaendelea kubaini iwapo vitasaidia katika kujua kilichosababisha ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG