Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:05

Wachunguzi wanaendelea kutafuta chombo cha kurekodi taarifa za ndege ya China iliyoanguka


Wachunguzi wakitoa taarifa za maendeleo ya kutafuta kifaa cha ndege iliyoanguka China (Picha AP Photo/ Ng Han Guan)
Wachunguzi wakitoa taarifa za maendeleo ya kutafuta kifaa cha ndege iliyoanguka China (Picha AP Photo/ Ng Han Guan)

Wachunguzi wa China, Alhamisi wamesema wanaendelea kufanya ukaguzi eneo la ajali la milimani kwa kifaa cha kurekodi taarifa za ndege ya China iliyoanguka Jumatatu kusini mwa jimbo la Guangxi.

Wakati huohuo maafisa wa mamlaka ya anga ya China wamesema licha ya kasha la nje la kifaa cha kurekodia sauti katika chumba cha marubani kuharibika, mkanda wake upo viruzi na wachuguzi wameanza kuufanyia kazi.

Ndege ya shirika la China, Eastern ilianguka ghafla na kugonga mlima nje ya mji wa Wazhou.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ilikuwa imebeba abiria 132 na wafanyakazi ikiwa safarini kutoka jimbo la Yunnan kwenda mji wa viwanda wa Guangzhou.

Taarifa kutoka mtandao wa ufuatiliaji wa safari za ndege wa Flight Radar 24, umeonyesha ndege ilidongoka kwa kasi ya mita 8,870 kwa dakika kabla ya kudondoka.

Mpaka sasa mabaki ya ndege na miili ya watu imepatikana na hakuna aliyepona licha ya kutotangazwa ramsi kwamba watu wote waliokuwemo wamefariki dunia.

XS
SM
MD
LG