Wakati akilihutubia taifa kutoka ikulu ya Nairobi Jumamosi, Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa kulegeza masharti kwa asilimia 20 huenda kutapelekea maambukizi mapya 200,000 na vifo 30,000 ifikapo Disemba. Rais, hata hivyo, amesema amri hiyo itaanza kutekelezwa kati ya saa tatu usiku hadi za kumi alfajiri kuanzia Jumapili.
Maambukizi
Mkuu wa nchi amesema kuwa kulegeza masharti kwa asilimia 40, kutasababisha maambukizi kufikia kileleni ifikapo Novemba na kukadiria kuwa kutakuwa na maambukizi 300,000 na vifo 40,000.
“Wakati janga hili likienea katika mataifa mbalimbali ulimwenguni, Kenya haijaepuka hili. Hatujawahi kukabiliwa na tishio la maslahi yetu ya kitaifa kwa kiwango hiki huko nyuma,” amesema Kenyatta.
Ameongeza kuwa : “ Familia zetu, shule zetu, maisha yetu, jinsi tunavyo abudu, uchumi wetu, biashara zetu, wafanyakazi wetu, kila raia wa Kenya anakabiliwa na hatari ya ugonjwa huu wa COVID-19 usioonekana, adui asiyerudi nyuma.”
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Nairobi.