Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 16:11

Kenya yakumbuka miaka kumi tangu mauaji ya Westgate mall


Wafanyikazi wa duka la Nakumatt wakisali kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa pili wa shambulio la jumba la maduka la Westgate huko Nairobi, Septemba 21 2015. Picha na SIMON MAINA / AFP.
Wafanyikazi wa duka la Nakumatt wakisali kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa pili wa shambulio la jumba la maduka la Westgate huko Nairobi, Septemba 21 2015. Picha na SIMON MAINA / AFP.

Imetimia miaka kumi tangu moja ya shambulio baya kuliko yote nchini Kenya, lililouwa watu 67 na kujeruhi wengine 200 katika eneo la maduka la westgate katika mji mkuu wa Nairobi Septemba 20, mwaka 2013.

Ilikuwa Jumamosi mchana wakati watu wenye silaha walipo vamia eneo hili la maduka lililokuwa limejaa watu na kuanza kushambulia kwa bunduki za rashasha na kurusha magruneti.

Watu hao wenye silaha walilishikilia eneo hilo kwa takriban saa 80, kabla ya vikosi vya usalama kuchukua udhibiti.

Miaka kumi baadaye, Loi Awat bado anakumbuka maombi ya kukata tamaa ya watu waliokuwa karibu naye wakati alipokuwa ameshikiliwa kwa siku nne katika eneo la maduka ya kifahari la Westgate.

Kwa saa nne za kutisha, Awat alijikunja chini ya meza ndogo katika ukumbi wa benki kwenye eneo hilo la maduka jijini Nairobi, ambako alikwenda kutoa pesa kwa ajili ya kuhudhuria mchezo wa rugby na binamu zake wawili.

Anasema kila kitu kilitokea katika sekunde moja.

Wanajeshi wa Kenya wakiwa wamejificha baada ya milio ya risasi karibu na jumba la Westgate huko Nairobi, Septemba 23 2013. Picha na CARL DE SOUZA / AFP.
Wanajeshi wa Kenya wakiwa wamejificha baada ya milio ya risasi karibu na jumba la Westgate huko Nairobi, Septemba 23 2013. Picha na CARL DE SOUZA / AFP.

"Nilisikia zogo nyuma yangu. Niligeuka nyuma na nilichokiona ni watu wanaokimbia. Sikuweza kuwaona binamu zangu," Awat aliliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano.

Anasema kuzungumzia matukio hayo ya kutisha yaliyotokea Septemba 21, 2013 kumemsaidia kupona.

Awat, ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 tu wakati huo na ndiyo kwanza amehitimu, anakumbuka kusikia milio ya risasi hewani, iliyomuacha akiwa amezubaa kwa hofu kwenye lango la benki.

"Mtu mmoja alinivuta chini kwenye sakafu na kwenye kona... Wazo langu la kwanza lilikuwa kwamba ulikuwa wizi wa benki."

Baada ya saa moja la kuchanganyikiwa, akituma ujumbe kwa familia na marafiki kwa hasira ili kujua kama kulikuwa na habari zozote za kile kilichokuwa kikitendeka katika jumba hilo la maduka, alisikia sauti zikiimba kiislamu "Allahu Akbar" zikitoka sehemu tano tofauti za maduka.

Wakati wa operesheni ya uokoaji katika shambulio la kigaidi la maduka ya Westgate, Septemba 21 2013. Picha na REUTERS/Noor Khamis.
Wakati wa operesheni ya uokoaji katika shambulio la kigaidi la maduka ya Westgate, Septemba 21 2013. Picha na REUTERS/Noor Khamis.

Kundi la wanajihadi lenye uhusiano na Al-Qaeda la Al-Shabaab lilidai kuhusika na tukio hilo, likisema lilikuwa likilipiza kisasi kwa jeshi la Nairobi lililoingilia Somalia.

Miaka miwili baada ya shambulio la Westgate, wapiganaji wa Al-Shabaab walishambulia Chuo Kikuu cha Garissa mashariki mwa Kenya, na kuua watu 148, wengi wao walikuwa wanafunzi.

Hilo lilikuwa shambulio la pili baya sana katika historia ya Kenya, lilishinda shambulio la Al-Qaeda katika ubalozi wa Marekani mjini Nairobi mwaka 1998, ambalo liliuwa watu 213.

Mwaka 2019, watu wenye bunduki wa kundi la Al-Shabaab waliwaua watu 21 katika hoteli ya Dusit jijini Nairobi mwaka 2019.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG