Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 08:49

Kenya na Haiti kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia


Rais wa Kenya William Ruto alipokuwa akihutubia kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Septemba 21, 2022. Picha na TIMOTHY A. CLARY / AFP.
Rais wa Kenya William Ruto alipokuwa akihutubia kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Septemba 21, 2022. Picha na TIMOTHY A. CLARY / AFP.

Haiti na Kenya zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia siku ya Jumatano. Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na majadiliano ya kimataifa kuhusu uwezekano wa Kenya kuongoza kikosi cha kimataifa cha usalama.

Kikosi ambacho kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuwasaidia polisi kupambana na ongezeko la vita vya magenge nchini Haiti.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huenda likapiga kura kwa ajili ya kikosi cha kimataifa kwa Haiti katika muda wa wiki moja, Brian Nichols, waziri mdogo wa Marekani katika masuala ya ukanda wa Magharibi, alisema katika mahojiano na Sauti ya Amerika wiki hii.

Serikali ya Ariel Henry iliomba msaada wa kimataifa kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba mwaka jana, lakini licha ya wito wa mara kwa mara kutoka Umoja wa Mataifa, ombi hilo halikujibiwa mpaka Kenya iliposema iko tayari kuongoza kundi la aina hiyo mwezi Julai.

Wakiwa na rasilimali chache, polisi wa Haiti wamekuwa wakipambana na magenge yenye nguvu ambayo sasa yanakadiriwa kudhibiti sehemu kubwa za nchi.

Rais wa Kenya William Ruto na Henry walishuhudia kutiwa saini kwa mkataba wa kuanzisha uhusiano huo katika misheni ya Kenya huko New York.

"Kama taifa linaloongoza katika ujumbe wa usalama unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Haiti, tumejitolea kupeleka timu maalum," Ruto alisema katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

Timu ingetathmini hali na kuandaa mikakati ya kuhakikisha masukuhisho ya muda mrefu, aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG