Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:46

Kampuni ya Uber yazindua bodaboda za umeme Kenya


Mfanyakazi katika kiwanda cha kuunganisha pikipiki za umeme huko Nairobi, Kenya Novemba 2, 2022. Picha na REUTERS/Monica Mwangi
Mfanyakazi katika kiwanda cha kuunganisha pikipiki za umeme huko Nairobi, Kenya Novemba 2, 2022. Picha na REUTERS/Monica Mwangi

Kampuni ya usafiri ya Uber Alhamisi imezindua huduma za pikipiki zinazotumia umeme nchini Kenya. Hii ni huduma ya kwanza barani Afrika, wakati kampuni hiyo ikijaribu kuingia katika jukwaa la kimataifa kuondoa uzalishaji wa hewa chafu ifikapo mwaka 2040.

Usambazaji wa pikipiki hizo nchini Kenya utafanyika baadaye mwaka huu katika nchi za Nigeria, Ivory Coast, Ghana, Uganda, Tanzania na Afrika Kusini, alisema meneja mkuu wa Uber katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara Afrika, Kagiso Khaole.

Madereva wataona gharama zao za uendeshaji zikishuka kwa kati ya asilimia 30 mpaka 35, na watumiaji watalipa asilimia 15 hadi 20 pungufu chini ya bei ya kawaida ya pikipiki ya Uber, kampuni hiyo ilisema.

Kenya, ambayo inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya nishati yake kutoka vyanzo mbadala, imekuwa ikijiweka kuwa kitovu kinachoongoza katika mabadiliko ya usafiri wa kijani katika bara la Afrika, awali kampuni ya Uber ilifanya majaribio madogo ya pikipiki hizo za umeme na washirika wa nje.

Ukuaji wa soko la magari ya umeme barani Afrika umepungua kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kutosha ya chaji za umeme na vifaa vinavyohusiana.

Rais wa Kenya William Ruto alisema mwezi uliopita kuwa, alitaka kuona idadi ya pikipiki za umeme zikiongezeka barabarani kutoka pikipiki 2,000 zilizopo havi sasa hadi kufikia zaidi ya pikipiki 200,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024.

Usafiri wa pikipiki ni mwajiri mkubwa nchini Kenya, unaovutia

mamilioni ya watu ambao wameshindwa kupata ajira rasmi.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG