Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 17:57

Deni la Taifa Kenya laongezeka kufikia shilingi trilioni 1.56


Muonekano wa Barabara ya Nairobi Expressway iliyojengwa na Shirika la Barabara na Madaraja la China (CRBC) Mei 8, 2022. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya
Muonekano wa Barabara ya Nairobi Expressway iliyojengwa na Shirika la Barabara na Madaraja la China (CRBC) Mei 8, 2022. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya

Kiwango cha deni la Kenya kimefikia kiwango cha juu licha ya Rais William Ruto kuapa kupunguza azma ya kuendelea kukopa, takwimu za Hazina zinaonyesha.

Jumla ya deni la taifa limepanda na kufikia rekodi ya shilingi trilioni 1.56 ambazo ni sawa na dola bilioni 10.8 katika mwaka wa fedha uliomalizika Juni 30 na kufikia shilingi trilioni 10.1, hivyo kuvuka ukomo wa deni wa shilingi trilioni 10, kulingana na data iliyotolewa Jumanne.

“Ongezeko la deni la taifa limechangiwa na malipo ya mikopo ya nje, kushuka kwa kiwango cha ubadilishaji fedha na malipo ya deni la ndani na nje,” Hazina ilisema.

Gharama za kurejesha mikopo, haswa kwa China, zimeongezeka wakati sarafu ya Kenya katika biashara ikiwa katika rekodi ya chini sana cha takriban shilingi 144 kwa dola moja.

Gharama ya kulipa madeni katika kipindi cha mwaka uliomalizika mwezi Juni ilikuwa shilingi bilioni 391 ambapo malipo ya juu zaidi -- shilingi bilioni 107 -- yalikwenda China.

Wabunge nchini Kenya walipiga kura mwezi Juni kubadilisha kiwango cha juu cha kukopa kutoka kile kilichopangwa hadi sehemu ya pato la taifa (GDP). Baraza la Seneti bado halijapitisha marekebisho hayo.

Ruto aliingia mamlakani mwaka jana akiahidi kufufua uchumi wa nchi ambayo ina takriban watu milioni 53.

Akieleza mpango wake wa mageuzi ya kiuchumi "kuanzia chini kwenda juu", Ruto aliahidi kupunguza deni la serikali na kuanzisha sera za kuweka pesa mifukoni mwa Wakenya ambao ni maskini.

Ukuaji wa uchumi ulipungua hadi asilimia 4.8 katika kipindi cha mwaka 2022 kutoka asilimia 7.6 mwaka uliopita, na unatabiriwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia tano mwaka huu, kulingana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG