Mfumo wa Worldcoin ambao ulianzishwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya OpenAl, Sam Altman, ulianza kufanya kazi mwezi Juni nchini Ujerumani na unawapa watumiaji utambulisho wa kibinafsi wa kidijitali, baada ya kukaguliwa sehemu ya macho yao iitwayo Iris.
Mradi huo kulingana na waanzilishi wake, unalenga kutatua moja ya changamoto kuu zinazokabili sekta ya crypto ambayo kwa kiasi kikubwa inatumia majina bandia ili kufanya kazi, na kuiweka katika hatari ya kutumiwa na matapeli.
Watumiaji waliojiandikisha katika mradi huo nchini Kenya walipewa tokeni 25 za bure za Worldcoin zenye thamani ya shilingi 7,000, na kuwavutia maelfu ya watu kwenye vituo vingi vya kujisajili katika mji mkuu Nairobi.
Waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki alisema mamlaka “zilitiwa wasiwasi” na mradi huo na zimeanzisha uchunguzi ili kubaini “usalama na ulinzi wa taarifa za siri zinazokaguliwa, na jinsi wakaguzi wanakusudia kutumia taarifa hizo”.
Forum