Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:00

Mahakama Kenya imeipa META siku 21 kutatua mzozo wao na walalamikaji


Logo ya Meta ambayo ni kampuni mama ya Facebook
Logo ya Meta ambayo ni kampuni mama ya Facebook

Wasimamizi wa maudhui 184 wanaishtaki Meta na wakandarasi wadogo wawili baada ya kusema walipoteza ajira  zao katika moja ya makampuni, Sama kwa kuunda umoja

Mahakama nchini Kenya imeipa kampuni mama ya Facebook, Meta na wasimamizi wa maudhui ambao wameshtaki kwa kuachishwa kazi bila ya haki, muda wa siku 21 kutatua mzozo wao nje ya mahakama, amri ya mahakama ilionyesha Jumatano.

Wasimamizi wa maudhui 184 wanaishtaki Meta na wakandarasi wadogo wawili baada ya kusema walipoteza ajira zao katika moja ya makampuni, Sama kwa kuunda umoja.

Walalamikaji wanasema walizuiwa kuomba nafasi hizo-hizo kwenye kampuni ya pili ya Majorel yenye makao yake Luxembourg baada ya Facebook kubadili wakandarasi.

Pande hizi zitatakiwa kuendelea kumaliza shauri lao nje ya mahakama kwa upatanishi ilisema amri ya Mahakama ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, ambayo ilisainiwa na wanasheria wa walalamikaji, Meta, Sama na Majorel.

Forum

XS
SM
MD
LG