Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:59

Iran yafafanua kilichokuwa kinawapa wasiwasi IAEA kuhusu eneo la vinu vya nyuklia


Rais wa Iran Ebrahim Raisi akisalimiana na mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi katika ofisi ya Rais, Tehran, Machi 4, 2023. (Iranian Presi, dency Office via AP)
Rais wa Iran Ebrahim Raisi akisalimiana na mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi katika ofisi ya Rais, Tehran, Machi 4, 2023. (Iranian Presi, dency Office via AP)

Iran na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki wamefikia makubaliano juu ya maswali yanayohusiana na moja ya meneo matatu ambako wakaguzi walikuta chembechembe za nyuklia ambazo hazikutolewa taarifa, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumanne.

IAEA kwa miaka kadhaa imekuwa ikitafuta majibu kutoka Iran kuhusu kile wakaguzi walichosema kuwepo kwa chembechembe za “madini ya uranium yenye asili ya anthropogenic.”

Mfululizo wa mikutano, ikiwemo ziara ya mkuu wa IAEA Rafael Grossi mwezi Machi huko Tehran ilipelekea ahadi iliyotolewa na Iran kutoa ushirikiano kwa uchunguzi huo.

Vyombo vya habari vya Iran vilisema Jumanne pande hizo mbili zilikuwa zimetatua suala la eneo la Marivan, ambalo liko jimbo la Fars.

Ripoti kadhaa za IAEA zilisema uchambuzi wa sampuli zilizochukuliwa kutoka katika eneo hilo mwaka 2020 zilionyesha kulikuwa na chembechembe za uranium. IAEA ilisema ilikuwa na taarifa kuwa mwaka 2003 Iran ilipanga kutumia na kuhifadhi malighafi za nyuklia katika eneo hilo kwa ajili ya majaribio ya vilipuzi.

Iran imekanusha madai hayo kwamba ilikuwa inajishughulisha na utengenezaji wa silaha za nyuklia,

Hofu ya kuwa Iran ina program ya silaha ilichochea mkataba wa 2015 ambao Iran ilisaini na Uingereza, China, Ufaransa, Russia, Marekani na Ujerumani ambao uliiwekea masharti programu ya nyuklia ya nchi hiyo kwa mabadilishano ya afueni ya vikwazo..

Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo mwaka 2018 kutokana na kile Rais wa wakati huo Donald Trump kusema msingi ya makubaliano hayo yalikuwa yanaipendelea Iran.

Iran ilijibu kwa kujiondoa kutoka katika ahadi zake chini ya makubaliano hayo, ikiwemo kusindika uranium kwa viwango vya juu, kuendeleza vinu vya kisasa vya nyuklia na kuhodhi kiwango kikubwa cha uranium iliyosindikwa.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG