Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:19

Israel yadai Iran sasa una uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia


Waziri wa ulinzi wa Israeli, Yoav Gallant .
Waziri wa ulinzi wa Israeli, Yoav Gallant .

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Alhamisi amesema kwamba Iran inaweza kuwa na uranium ya kutosha kwa ajili ya silaha tano za nyuklia, na kuionya Tehran kwamba kuendelea kutengeneza silaha hizo kutaweza kusababisha maafa katika kanda hiyo.

Matamshi yake yanaunga mkono wasiwasi wa kimataifa ambao umeongezeka katika miezi kaadhaa iliyopita kwamba Tehran inafikia karibu kiwango cha uraniam cha kuwa na silaha kuliko muda wowote.

Wataalamu wanasema Jamuhuri hiyo ya Kislamu ina mafuta ya kutengeneza mabomu ya atomik kama itaamua kufanya hivyo.

Utawala wa Israel unatoa mwito kwamba Iran inaweza kuzuiwa tu kutengeneza silaha za nyuklia kwa vitisho vya kuchukuliwa hatua za kijeshi, huku Marekani kwa uwazi inaunga mkono kurejea kwenye juhudi za kidiplomasia za mataifa mengi.

Shirika la kimataifa la nguvu za atomik lilisema mwezi Machi kwamba litaanza tena ukaguzi na kuwaka kamera za uangalizi kwenye vituo vya nyuklia vya Iran baada ya kuripotiwa uwepo wa kiwango kikubwa cha uranium chini ya ardhi kwenye maeneo ya nyuklia.

XS
SM
MD
LG