Hakukuwa na taarifa kuhusu uharibifu wowote katika mlipuko huo.
Shirika la habari la serikali la IRNA limesema mlipuko huo ulitokea wakati wa usafirishaji wa risasi kwenye kituo cha walinzi nje kidogo ya mji wa Damghan, kaskazini mwa mkoa wa Semnan.
Ripoti hiyo haikutoa maelezo mengine kuhusu chanzo cha mlipuko huo.
IRNA ilielezea pia tukio hilo lilikuwa likifanyiwa uchunguzi.
Shirika la habari lisilo rasmi kabisa la Fars lilisema kwenye kituo chake cha Telegram kwamba wafanyakazi wawili waliuwawa na watatu wengine walijeruhiwa.