Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:07

Iran na Taliban wanafanya mazungumzo kumaliza uhasama na mgogoro wa maji


Mapigano yalitokea kwenye jimbo la mpakani la Nimroz, Afghanistan, jana jumamosi na kupelekea vifo vya maafisa wa wawili wa usalama wa Iran na mlinzi wa mpakani wa Taliban.

Pande zote mbili zimelumiana kufuatia mapigano hayo ya mpakani ambayo yameongeza mivutano kati ya Iran na Afghanistan kuhusu matumizi ya maji.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Afghanistan amesema kwamba serikali yake haitaki kupigana na majirani zake, akisistiza kwamba wanajeshi wa Iran ndio walioanza mapigano.

Mivutano kati ya Afghanistan na Iran imekuwa ikiendelea, Iran ikidai kwamba Taliban wamekuwa wakikiuka makubaliano ya mwaka 1973 kati ya Tehran na Kabul kuhusu matumizi ya maji ya mto Helmand unaotoka Afghanistan kuelekea mashariki mwa Iran.

Forum

XS
SM
MD
LG