Washukiwa hao wote ambao wametajwa kama wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya wenye silaha walikuwa wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa katika hukumu iliyoidhinishwa na mahakama ya juu ya Iran, tovuti ya mahakama ya Mizan Online ilimnukuu Mojtaba Ghahramani, Jaji Mkuu wa jimbo la kusini la Hormozgan.
Mojtba aliongeza kusema kwamba hukumu za watu waliotajwa zilitekelezwa asubuhi ya Jumatatu katika magereza ya Bandar Abbas na Minab ya Hormozgan.
Idadi ya sasa ya kunyongwa watu hao inafikia wanane ambapo ni idadi ya watu waliouawa katika kipindi cha chini ya wiki moja kutokana na ulanguzi wa dawa za kulevya.