Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:44

IMF iko tayari kuisaidia Kenya


Rais wa Kenya William Ruto (kulia) akicheka na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga, Juni 23, 2023 huko Paris, Ufaransa. Picha na Lewis Joly/ REUTERS.
Rais wa Kenya William Ruto (kulia) akicheka na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga, Juni 23, 2023 huko Paris, Ufaransa. Picha na Lewis Joly/ REUTERS.

Shirika la kimataifa la fedha duniani (IMF) litafanya "kila linalowezekana" kuisaidia Kenya, Mkurugenzi wa shirika hilo, Kanda ya Afrika Abebe Selassie alisema Ijumaa, wakati wafanyakazi wake wanatarajiwa kuitembelea nchi hiyo ya Afrika Mashariki wiki ijayo.

Gavana wa benki kuu ya Kenya aliliambia shirika la habari la Reuters wiki hii kuwa Kenya imekuwa ikifanya majadiliano na IMF juu mpango wake wa mkopo, ikiwezekana kwa kuomba ufadhili kwa "fursa ya kipekee” Kamau Thugge pia alisema Kenya inapanga kununua hadi robo ya bondi za kimataifa zenye thamani ya $2 bilioni mwaka 2024 baada ya kupata mikopo mipya.

Ikiwa itapewa "fursa ya kipekee" Kenya inaweza kuomba

kwa zaidi ya ukomo wake wa ufadhili wa IMF.

"Tumetiwa moyo sana kwamba serikali (ya Kenya) inafanya kazi kwa bidii ...... kwa njia mbadala mbali mbali ili kushughulikia muda wa mwisho ambao unaangukia mwaka ujao,” Selassie aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Marrakech katika Mikutano ya Mwaka ya IMF na Benki ya Dunia.

“Kwa nchi zinazoendelea kutekeleza sera kama ilivyokusudiwa, ambazo zinazisukuma sera katika mwelekeo sahihi, sisi tufanye tunachoweza kuwapatia ufadhili wanaohitaji."

Wakati huo huo wakuu wa IMF na Benki ya Dunia waliyasihi mataifa wanachama siku ya Ijumaa kuongeza nguvu ya ufadhili wa wakopeshaji wa kimataifa ili kuzisaidia nchi maskini sana kukabiliana na umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa.

Walitoa maombi yao katika mazungumzo ya wiki moja ya mawaziri wa fedha duniani na magavana wa benki kuu huko Marrakesh, Morocco -- mikutano ya kwanza ya kila mwaka ya IMF-Benki ya Dunia katika ardhi ya Afrika tangu 1973.

Chanzo cha taarifa hii inatoka shirika la habari la AFP and Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG