Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:59

Mahakama Kenya yahalalisha uagizaji na matumizi ya chakula cha GMO


Ulimaji wa nafaka ya GMO nchini Kenya.
Ulimaji wa nafaka ya GMO nchini Kenya.

Mahakama nchini Kenya imehalalisha uagizaji na ukuzaji wa chakula cha GMO, hatua hii ikipuuzia kesi iliyowasilishwa na chama cha mawakili nchini humo.

Katika uamuzi wake Mahakama ya Mazingira Kenya inasema waliowasilisha kesi hiyo walishindwa kutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Chakula cha GMO ni hatari kwa matumizi ya binadamu.

Uamuzi wa Jaji Oscar Angote umetupilia mbali madai kuwa kabla ya kuidhinishwa matumizi ya chakula hicho nchini humo, zoezi halikufanyika la kuwashirikisha wananchi ambapo ni kwa mujibu wa katiba.

Badala yake mahakama hiyo ilisema taarifa hiyo ya kuwashirikisha wananchi ilichapishwa kwenye gazeti la serikali.

Chama cha mawakili nchini humo kiliwasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya serikali ya Rais William Ruto ya kuidhinisha uagizaji wa chakula cha GMO nchini humo kwa madai si salama kwa matumizi ya binadamu.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Zainab Said, Kenya

Forum

XS
SM
MD
LG