Haikusema imeongeza watumiaji wangapi kama matokeo ya mpango huo, uliobuniwa ili kusaidia kusajili watumiaji wapya watakaolipa.
"Kwa kweli tumejifunza mengi kutokana na jaribio hilo," msemaji wa Netflix ililiambia shirika la habari la Reuters, bila kutoa maelezo. "Tutaendelea kutoa mipango mingi tofauti.
"Netflix inazindua mpango utakaosaidiwa na matangazo, kuwapa wateja huduma ya kulipa dola 6.07 kwa mwezi, lakini msemaji huyo hakuzungumzia upatikanaji wa huduma hiyo nchini Kenya.
Ingawa uchumi wa nchi kama kenya yenye kipato cha kati cha chini, utoaji wa huduma za utiririshaji ni fursa kubwa ya kukuza idadi ya wateja, pia kunaleta changamoto wakati nguvu ya ununuzi imepungua kutokana na mfumuko wa bei, watendaji wa tasnia walisema.
Chini ya mpango wa bila malipo, ambao utamalizika tarehe moja Novemba, watazamaji walikuwa na uwezo wa kutazama vipindi vilivyotayarishwa na nchi za Magharibi kama vile "Money Heist" na "Bridgerton," na zile za Kiafrika kama "Damu na Maji."
Netflix imekuwa ikitoa maudhui zaidi ya nyumbani kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kama sehemu ya mkakati wake wa kuwapata watumiaji wapya katika bara hilo. Pia imekuwa ikifanya ushirikiano na kampuni za simu za ndani ili kurahisisha malipo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters
Forum