Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:46

ICRC: Kuimarika kwa usalama Tigray kwarahisisha ufikishaji misaada ya dharura


Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ikipeleka misaada katika maeneo yaliyoathiriwa na vita huko Tigray.
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ikipeleka misaada katika maeneo yaliyoathiriwa na vita huko Tigray.

Kuimarika kwa usalama katika mkoa wa  Tigray nchini Ethiopia tangu sitisho la  mapigano lililofikiwa mwezi Novemba kumeruhusu misaada kwenda kwenye baadhi ya maeneo ambayo hapo awali yalikuwa hayafikiwi...

Kuimarika kwa usalama katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia tangu sitisho la mapigano lililofikiwa mwezi Novemba kumeruhusu misaada kwenda kwenye baadhi ya maeneo ambayo hapo awali yalikuwa hayafikiwi, lakini mahitaji ya kibinadamu bado ni ya dharura, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilisema.

Vita vya miaka miwili vilivyozuka Novemba 2020, kati ya serikali na majeshi yanayoongozwa na chama kinacho tawala eneo hilo, Tigray People’s Liberation Front (TPLF), viliua maelfu ya watu, na kuwasababisha hali ya njaa kwa maelfu na mamilioni ya watu kukoseshwa makazi.

Serikali na vikosi vya Tigray walikubaliana kumaliza uhasama mwezi Novemba , ambapo misaada ya ziada iliruhusiwa kuingia katika mkoa huo na kwa baadhi ya huduma kurejeshwa. Hata hivyo, uharibifu wa hospitali na uporaji wa magari ya wagonjwa wakati wa vita inamaanisha huduma za matibabu bado zinakosekana, ICRC ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyoambatanishwa na na picha mpya za vituo vya afya vya eneo hilo.

Kiongozi wa mazungumzo ya usuluhishi Getachew Reda akiongea kwa simu katika mazungumzo ya amani mjini Nairobi, Kenya Nov 12, 2022.
Kiongozi wa mazungumzo ya usuluhishi Getachew Reda akiongea kwa simu katika mazungumzo ya amani mjini Nairobi, Kenya Nov 12, 2022.

Kati ya magari ya wagonjwa 250 ambayo yalikuwa yanatumiwa na chama cha msalaba mwekundu nchini Ethiopia kabla ya mzozo ni 82 tu yamebaki na idadi kubwa hayafanyi kazi ICRC ilisema.

Waziri wa afya wa Ethiopia Lia Tadesse, mshauri wa uslama wa taifa wa waziri mkuu Redwan Hussein, na msemaji wa vikosi vya Tigray Getachew Reda hawakutoa majibu ya haraka kuhusu hali ya kibinadamu.

XS
SM
MD
LG