Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:17

Timu ya ngazi ya juu Ethiopia inaelekea Mekele kwa mazungumzo na waasi


Waandamanaji nchini Ethiopia wakitoa wito wa kusitisha mapigano nchini mwao
Waandamanaji nchini Ethiopia wakitoa wito wa kusitisha mapigano nchini mwao

Miongoni mwa vipengele vya makubaliano hayo ni kuweka utaratibu wa ufuatiliaji na utekelezaji ili pande zote mbili ziweze kuwa na imani kuwa sitisho la mapigano linaheshimiwa na ukiukwaji wowote unashughulikiwa

Timu ya ngazi ya juu ya Ethiopia ilikuwa njiani Jumatatu kuelekea mkoa unaoshikiliwa na waasi wa Tigray kwa mazungumzo juu ya utekelezaji wa makubaliano ya amani ili kumaliza mzozo uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Addis Ababa na vikosi vya waasi wa Tigray wamekubaliana kuunda chombo cha pamoja cha ufuatiliaji ili kuhakikisha makubaliano ya amani ya mwezi Novemba ya kumaliza vita vya kikatili yanaheshimiwa na pande zote.

Miongoni mwa vipengele vya makubaliano hayo ni kuweka utaratibu wa ufuatiliaji na utekelezaji ili pande zote mbili ziweze kuwa na imani kuwa sitisho la mapigano linaheshimiwa, na ukiukwaji wowote unashughulikiwa.

Maelfu ya watu wamekufa katika kipindi cha miaka miwili ya umwagaji damu katika jimbo la Tigray.

"Ujumbe huo ni wa kwanza wa ngazi ya juu wa serikali kuu kuelekea Mekele katika kipindi cha miaka miwili," taarifa ilisema, na kuongeza kuwa ujumbe uliongozwa na spika wa Baraza la Wawakilishi, Tagesse Chafo.

Lengo ni kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini Novemba 2.

XS
SM
MD
LG