Polisi wa serikali kuu, “kulingana na mamlaka waliyopewa na katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia kulinda taasisi za serikali kuu” waliingia Mekele na kuanza kazi,” idara yao imesema katika taarifa kwenye Facebook.
“Watatoa usalama wa kutosha kwa taasisi zinazosimamiwa na serikali kuu, ikiwemo viwanja vya ndege, nishati ya umeme, huduma za mawasiliano ya simu, benki na taasisi nyingine zinazotoa huduma za umma.”
Vita kati ya serikali kuu ya Ethiopia na Tigray vilianza mwezi Novemba mwaka 2020. Waziri mkuu Abiy Ahmed alipeleka wanajeshi ndani ya jimbo hilo la kaskazini baada ya kukishtumu chama tawala katika jimbo hilo, Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kushambulia kambi za jeshi la Ethiopia.
Makadirio kuhusu vifo yanatofautiana sana, huku Marekani ikisema watu nusu milioni waliuawa katika vita hivyo.